Friday, February 7, 2014

UFUGAJI WA SAMAKI KWENYE BWAWA

Ufugaji wa samaki kama ilivyoshughuli nyingine yoyote ya kiuchumi inahitaji usimamizi  mzuri ili uweze kuwa na faida,mbali na hivyo mfugaji wa samaki anatakiwa kuzingatia vigezo vingi kabla hajaanza ufugaji.
Maji
Upatikanaji wa maji na ubora wake ni kigezo muhimu  katika ufugaji wa samaki.Mtiririko wa maji ni njia rahisi kwa mfugaji,Maji machafu hayatakiwi kwa ufugaji wa samaki wafugaji ni lazima wasaidiwe na maafisa kilimo katika eneo lao kama maji yanayopatikana yana ubora kwa ajili ya ufugaji wa samaki
Bwawa(Ponds)
Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia
Hii ni njai rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa .
Utunzaji wa Bwawa
Inashauriwa kufanyia bwawa usafi mara kwa mara hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki.
Pia ukiacha mimea bwawani itatumia virutubisho kwa kiasi kikubwa na kuondoa hewa ya oxijeni.
Ulishaji
Wafujaji walio wengi  wamekuwa hawazingatii kanuni za ulishashaji wa samaki .Kwa kawaida inatakiwa kuwalisha mara mbili hadi mara tatu kwa siku.
Aina ya Chakula
Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi ,mashudu ya pamba na alizeti,soya,mabaki ya dagaa.Haishauriwi kulisha chakula kilichoko kwenye mfumo wa vumbi bali kiwe mabonge madogo madogo kwa wastani wa tambi.
Magonjwa
Kwa kawaida samaki hawana magonjwa mengi sana yanayowashambulia ila kuna baadhi ya yaliyozoeleka kama vile magonjwa ya ukungu(Fangasi)magonjwa yatokanayo na virusi pamoja na minyoo.
Samaki wanaposhambuliwa na fangasi huonekana kwa macho kwa kuwa na madoa madoa .
Samaki aina ya kambale hushambuliwa zaidi kuliko perege pia unaweza kutambua kuwa samaki ni mgonjwa kwakuwa huzubaasehemu moja kwa muda mrefu
Magonjwa ya samaki pia yanaweza kutokana na mrundikano wa kwenye bwawa .Hivyo ni muhimu kuwapunguza kila wanapoongezeka.
Tiba
Tibaya iliyozoeleka kwa samaki ni kwa kuweka chumvi kwenye maji kisha kuwatumbukiza samaki unaowaona kuwa ni wagonjwa kisha kuwatoa na kuwarudisha bwawani.
Upatikanaji
Unaweza kupata vifaranga wa samaki kutoka katika kituo cha kuzalisha na kufuga samaki kingolwira morogoro .bei ya kifaranga cha pegere ni shilingi 50Tsh  na kambale ni shilingi 150Tsh

3 comments:

  1. asanten nimejifunza mengi juu ya samaki na umwanga nliyoupata lazima ni utumie kwan hadi sasa nishachimba bwawa na nipo katika changamoto ya upataji vifaranga wa samaki aina ya tilapia(sato)...... nipo mwanza naomba msaada wenu ya wapi nitapata vifaranga.

    ReplyDelete
  2. nahitaji kufuga samaki katika nyumba iliyopo iringa maeneo ya Lugalo-Mbigili,eneo nililonalo ni mita tano kwa saba,bwawa ni la kujenga kwa saruji,nataka kufuga sato. je inawezekana kufuga kwa maji ya bomba na je kutakuwa na ufanisi wowote au matatizo gani nianayoweza kukabibiliana nayo kwa ufugaji huo

    ReplyDelete
  3. Samaki wangu wanskufa mmoja mmoja kila siku hawanadalili yoyote zaid ya weupe na mukusi kidogo kwenye matamvua

    ReplyDelete