Wednesday, October 15, 2014

NAMNA KILIMO CHA TUMBAKU KINAVYOATHIRI MISITU SHINYANGA




KILIMO CHA TUMBAKU KINAVYOSABABISHA UKATAJI WA MITI OVYO.
Tumbaku  ni zao la kibishara linalolimwa na kuvunwa ili kutengeneza sigara,kwa mkoa shinyanga zao hili linalimwa kwa wingi wilayani kahama mkoa wa shinyanga.Ambalo pia nizao linaloongoza kwa mapato wilayani kahama ikifatiwa na madini(Dhahabu) yapatikanayo wilayani hapo.
Zao hili baada ya kuvunwa majani yake hukaushwa kwa kutumia majiko yenye kutumia kuni nyingi wakati wa kukausha tumbaku kabla ya kupaki na kuuza kwenye makampuni yanayonunua tumbaku kama ATTT, ALIANCE nk.
Namna tumbaku inavyochangia uharibifu wa misitu:
Baada ya kuvunwa kwa zao hilo la tumbaku wakulima wote hurudisha fikra zao katika msistu wa ushetu ubagwe ulioko wilaya ya ushetu( kahama)mkoa washinyanga ilikupata kuni kwa ajili ya kukaushia tumbaku na badala ya kuvuna kuni wao hutumia fursa hiyo kukata miti mikubwa kwaajili ya kukausha tumbaku pamoja na kuchana mbao kwa ajili ya biashara kinyume na sharia

            

Hii nimitiilyokatwa na kufanywa mbao

Huu ni msitu wa Ushetu Ubagwe ulioko katika wilaya ya Ushetu (Kahama) na hiyondiyo baadhi ya miti inayoendelea kuvunwa na wakulima wa tumbaku ilikupata kuni za kukaushia tumbaku .
Hili ni shimo linalotumika kuchania mbao yaliyochibwa msituni






Thursday, August 28, 2014

KILIMO CHA UYOGA HAKIHITAJI MAJI MENGI

Uyoga ni mazao yanayozalishwa kutokana na mimea iliyovunda .Mmea huu hauna uwezo wa kujitengenezea chakula chake mwenyewe kama ilivyo kwa mimea mingine kama vile ngano na mchele.
Upatikanaji wa uyoga huhitaji yafuatayo:
  • Maandalizi ya mbolea
  • upatikanaji wa mbegu
  • Mifuko ya kupandia
Aina za Uyoga
Uyoga upo wa aina mbalimbali ambapo kuna uyoga kwa ajili ya chakula na uyoga usioliwa baadhi ya uyoga unaopatikana Tanzania ni pamoja na
  • Oyster(Plerotus)
  • Button(Agricus)
  • Shitake(Lentinula edodes)
  • Chinese Mushroom(Ganoderma)
Faida ya kuotesha uyoga pamoja na mazao mengine ya biashara
  1. Haina Gharama ya eneo
  2. Hukua haraka (Muda wa kuotesha hadi kuvuna ni siku 28-35tu)
  3. Matumizi ya taka zinatokana na kilimo kwa ajili ya uzalishaji kama miwa,ndizi,majani,nyuzi,mahindi,maharagwe,na majani ya ngano.

Friday, February 7, 2014

UFUGAJI WA SAMAKI KWENYE BWAWA

Ufugaji wa samaki kama ilivyoshughuli nyingine yoyote ya kiuchumi inahitaji usimamizi  mzuri ili uweze kuwa na faida,mbali na hivyo mfugaji wa samaki anatakiwa kuzingatia vigezo vingi kabla hajaanza ufugaji.
Maji
Upatikanaji wa maji na ubora wake ni kigezo muhimu  katika ufugaji wa samaki.Mtiririko wa maji ni njia rahisi kwa mfugaji,Maji machafu hayatakiwi kwa ufugaji wa samaki wafugaji ni lazima wasaidiwe na maafisa kilimo katika eneo lao kama maji yanayopatikana yana ubora kwa ajili ya ufugaji wa samaki
Bwawa(Ponds)
Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia
Hii ni njai rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa .
Utunzaji wa Bwawa
Inashauriwa kufanyia bwawa usafi mara kwa mara hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki.
Pia ukiacha mimea bwawani itatumia virutubisho kwa kiasi kikubwa na kuondoa hewa ya oxijeni.
Ulishaji
Wafujaji walio wengi  wamekuwa hawazingatii kanuni za ulishashaji wa samaki .Kwa kawaida inatakiwa kuwalisha mara mbili hadi mara tatu kwa siku.
Aina ya Chakula
Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi ,mashudu ya pamba na alizeti,soya,mabaki ya dagaa.Haishauriwi kulisha chakula kilichoko kwenye mfumo wa vumbi bali kiwe mabonge madogo madogo kwa wastani wa tambi.
Magonjwa
Kwa kawaida samaki hawana magonjwa mengi sana yanayowashambulia ila kuna baadhi ya yaliyozoeleka kama vile magonjwa ya ukungu(Fangasi)magonjwa yatokanayo na virusi pamoja na minyoo.
Samaki wanaposhambuliwa na fangasi huonekana kwa macho kwa kuwa na madoa madoa .
Samaki aina ya kambale hushambuliwa zaidi kuliko perege pia unaweza kutambua kuwa samaki ni mgonjwa kwakuwa huzubaasehemu moja kwa muda mrefu
Magonjwa ya samaki pia yanaweza kutokana na mrundikano wa kwenye bwawa .Hivyo ni muhimu kuwapunguza kila wanapoongezeka.
Tiba
Tibaya iliyozoeleka kwa samaki ni kwa kuweka chumvi kwenye maji kisha kuwatumbukiza samaki unaowaona kuwa ni wagonjwa kisha kuwatoa na kuwarudisha bwawani.
Upatikanaji
Unaweza kupata vifaranga wa samaki kutoka katika kituo cha kuzalisha na kufuga samaki kingolwira morogoro .bei ya kifaranga cha pegere ni shilingi 50Tsh  na kambale ni shilingi 150Tsh

TESTIMONIES

Miss Nyangi Magoko
Nashukuru sana kituo cha Maarifa Centre kwa kunipatia mafunzo ya kompyuta kwani baada ya kuhitimu mafunzo hayo kwa ngazi ya cheti(Certificate)sasa nimejiunga na chuo cha ICT kilichopo mwanza na ninafanya Diploma ya ICT hivyo nawaomba vijana wenzangu wakitumie kituo hiki cha Maarifa Centre kwani kinapunguza idadi ya vijana waishio mitaani bila shughuli yoyote na hivyo kuboresha maisha ya jamii yote kwa ujumla.
Maarifa Centre ooooooyeeeeeeeeeeeeee!!!!

Tuesday, October 15, 2013

Shinyanga Maarifa centre Sub branch publicised on Dira Newspaper

On 7th-13rd of October 2013 were visited at Kinaga Maarifa centre to see the progress of Centre located at Kahama district 12 kilometre away from kahama town and to be published on Dira Newspaper but still we have a challenge on power so that we can run the equipment we have at centre computers and other machine .
That is newspaper logo
CKF of Kinaga Maarifa centre arranging the machine at Kinaga Maarifa.

FARMERS EXCHANGE VISIT

Shinyanga Maarifa centre were visited the farmer of Songambele Maarifa located at Kongwa district in Dodoma region ,Ten members were visit at Songambele (Advisory committee and Focal group) and the aim was to share experiance of what the farmers from two sides are doing (Shinyanga and Songambele) and capacity building for the Songambele Advisory committee .
During our tour we learn there is huge opportunities from songambele community in Honey processing and Sunflower cultivation which are popular produced at Songambele and Dodoma in general as Region.
The team from shinyanga were encouraged the farmer of Songambele to try on  Pad production by using water harvest like what Shinyanga Farmers doing and the team was lifted the pad seed at Maarifa Centre  to ensure the Field officer of Songambele prepare a demonstration plot for pad production  .
Songambele community were very interested on pad production which was not applicable ever since.
Mr Emmanuel Magoso showing the pad seed to songambele community during meeting
Songambele community members at Somgambele Maarifa centre during meeting.


Monday, September 9, 2013

Testimonies

Esther Makono:
Nashukuru sana kituo cha maarifa centre kwa mafunzo waliyotupatia ya computer bila gharama yoyote ambapo binafsi yameniwezesha kujua namna ya kuitumia kompyuta na kuniwezesa kutembelea tovuti mbalimbali hasa  zihusuzo mambo ya muungu kupitia kanisa letu la Mashahidi wa Yehova(Yehova Witness) mafunzo haya ni gaharama kubwa kuyapata kupitia vyuo vyetu vinavyotoa mafunzo haya ya kompyuta jambo ambalo lilinifanya nishindwe kumudu gharama hizo kutokana na kuwa na watoto wanaosoma vyuoni ambao pia wanahitaji pesa ili waweze kuendelea na masomo yao ,lakini kupitia kituo cha maarifa ambacho kinatoa huduma zake bure nimeweza kupata mafunzo hayo katika program zifuatazo ambazo ni microsoft word,Excel,Power Point pamoja na Internet nashukuru sana.