Thursday, August 28, 2014

KILIMO CHA UYOGA HAKIHITAJI MAJI MENGI

Uyoga ni mazao yanayozalishwa kutokana na mimea iliyovunda .Mmea huu hauna uwezo wa kujitengenezea chakula chake mwenyewe kama ilivyo kwa mimea mingine kama vile ngano na mchele.
Upatikanaji wa uyoga huhitaji yafuatayo:
 • Maandalizi ya mbolea
 • upatikanaji wa mbegu
 • Mifuko ya kupandia
Aina za Uyoga
Uyoga upo wa aina mbalimbali ambapo kuna uyoga kwa ajili ya chakula na uyoga usioliwa baadhi ya uyoga unaopatikana Tanzania ni pamoja na
 • Oyster(Plerotus)
 • Button(Agricus)
 • Shitake(Lentinula edodes)
 • Chinese Mushroom(Ganoderma)
Faida ya kuotesha uyoga pamoja na mazao mengine ya biashara
 1. Haina Gharama ya eneo
 2. Hukua haraka (Muda wa kuotesha hadi kuvuna ni siku 28-35tu)
 3. Matumizi ya taka zinatokana na kilimo kwa ajili ya uzalishaji kama miwa,ndizi,majani,nyuzi,mahindi,maharagwe,na majani ya ngano.

1 comment:

 1. Habari za kazi,mimi ni memba mpya na nilivutiwa na hii habari ya uyoga,sasa naitaji mbegu za uyoga aina ya oyster.Mimi nipo karagwe-kagera na E-mail yangu ni nalusaka@gmail.com

  ReplyDelete