Tuesday, April 17, 2012

 Library and Access point
 ICT training chamber and the training is proceeding .
Huu ndio muonekana wa kituo cha Maarifa centre ndani ya kituo chetu kwani tumetenganisha sehenu ya kuendeshea mafunzo ya kompyuta(ICT training) na Access point (sehemu ya huduma ya internet) na huu ndio muonekano wake.Mabadiliko haya yamefanywa kwa ushirikiano wa The Team from ALIN akiwemo Noah Lusaka( Project Manager),Kibe na Tonny bila kumsahau Msimamizi wa kituo (FIELD OFFICER) .
Willison Malongo  (Aliyevaa Kofia ):mafunzo ya kompyuta ni mazuri sana na yamenisaidia katika kuboresha kazi yangu na sasa hivi nafundisha wanafunzi wa chuo cha Uwalimu SHYCOM kozi ya Kompyuta hivyo basi sio tu nimejifunza kutumia kompyuta badala yake nimepata kazi ya kufundisha kwani pamoja  na hali yangu ya kutumia mkono mmoja sikukata tamaa na ninaishi na kufanya kazi kama mtu mwingine aliye na viungo vyake vyote.Nashukuru sana Kituo cha Shinyanga Maarifa Centre kwa kutupatia elimu  hii ya kompyuta tena bila gharama yoyote .Bila kuwasahau ALIN TEAM iliyokuja wanaoendelea kusaidia vifaa vya kufundishia zikiwemo Computer(IVENNO).
Kifo cha Muigizaji nguli wa Tanzania Marehemu Steven Charles Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia jumamosi ya tarehe  07.04.2012 amezikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar-esalam siku ya 10.04.2012.
Marehemu Kanumba alizaliwa 08.01.2012 katika hospitali ya mkoa wa shinyanga alisoma shule ya msingi Bugoi iliyoko shinyanga njini kilometa 5 kutoka kituo cha maarifa centre na badae kujiunga na shule ya sekondari Mwadui Sekondari ndipo alipohamia jijini Dar-esalam na kujiunga na kituo cha mafunzo ya sanaa KAOLE GROUP ndipo maisaha ya uigizaji ya Marahemu Kanumba .Steven Kanuba anefariki akiwa na umri wa miaka 28 hadi mauti imekuta hajaacha mke wala mtoto.Filamu zitakazo kumbukwa na pamoja na Uncle JJ,
Young Billionaire,King of Devil .nk Kiukweli ni pigo kwa nhi ya Tanzania na Kwa tasinia ya Sanaa nchini Tanzania  je wewe unamjuaje Marehemu Steven Kanumba?????????????????  
Moja kati ya huduma zitolewazo kwa jamii bila gharama yoyote ni pamoja na huduma ya Maktaba hii imetokana na mahitaji ya wakazi wa Shinyanga walioko karibu na Kituo cha Maarifa Centre na kituo hiki kimesaidia wanafunzi wa chuo cha afya (HEALTH COLLAGE) kilichopo Kolandoto Shinyanga nje kidogo umbali wa kilometa 15 kutoka Kituo cha Maarifa Centre.
Henri Thomas (21)ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho ametumia kituo chetu hasa kujisomea vitabu tulivyonavyo ambavyo tuho navyo na amefaulu katika somo ambalo alikuwa linamsumbua (ANATOMY) ambalo alikuwa akipata alama 56% hadi 85%.

Hakuna kitu kinachoshindikana katika ulimwengu wa kompyuta kwani hata mzee Willison Malongo(56) huyu mwenye ulemavu wa mkono amejifunza kompyuta na  anaweza kutumia kompyuta tena kuliko mtu asiye na ulemavu.na amepata kazi ya kufundisha kompyuta katika chuo cha walimu shinyanga(SHYCOM).