Friday, August 24, 2012

AKINA MAMA WAKIWA WANATENGENEZA MPUNGA KATIKA KIJIJI CHA BULIMA WAKATI NIMEENDA KUTEMBELEA VIKUNDI VYA KINAMAMA

MISS LEAH AKIFATILIA MAFUNDI WANACHOKIFANYA

JIKO SANIFU LINALOTUMIA KUNI MBILI TU

NAMNA JIKO SANIFU LINAVYO ANZA KUJENGWA NA HAO NDIYO MAFUNDI(LOCAL ARTISAN)

Jiko sanifu ni moja kati ya mikakati ya kupunguza matumizi ya vyanzo vikubwa vya nishati kwani jiko hili linatumia kuni mbili tu(firewood) kwa kupika chakula na kikaiva hivyo basi kwa  mtu anayetumia jiko hili sanifu(IMPROVE COOK STOVE) atatumia kuni tano tu kwa siku . hivyo basi ili tuweze kuondikana na uharibifu wa misitu na ukataji wa miti ovyo tembelea kituo chetu cha maarifa centre kwa ushauri na maelezo zaidi juu ya matumizi na faida ya kutumia jiko sanifu.
 Lakini moja kubwa ni kupunza vifo vya akina mama wanaotumia mafiga matatu yanayowasababishia macho kuwa mekundu na kuuitwa wachawi hadi kupelekea kuuwawa kikatili kwa imani za kishirikina.
Ona kina mama hawa wanatumia majiko sanaifu wakiwa wanatengeneza mazao ili wakapike wakiwa wamejaa furaha.

SENSA YA WATU NA MAKAZI INATARAJIWA KUANZA TAREHE 26.AUGUST.2012 HADI 2.SEPTEMBA 2012

Tanzania inatarajia kuhesabu watu na makazi yao ili kupata takwimu za wananchi wote walioko nchini (TANZANIA) ili kupanga maendeleo yanayo endana na idadi ya watu walioko nchini .
Hivyo basi watu wote waliokoTanzania na wasio raia wa Tanzania watahesabiwa .
Sensa kwa maendeleo ya Taifa wananchi wote mnaombwa kutoa ushirikiano wenu kwa makarani wa sensa.

MAFUNDI WASHI WAKIWA WANACHANGANYA MCHANGA NA CEMENT

MTAMBO WA BIOGAS(BIOGESI)

Ni moja kati ya majiko ambayo shinyanga maarifa centre mtambo unaotumia kinyesi cha ng'ombe ambao baada ya kutengeneza gesi mtambo huu unaweza kuwasha taa tatu 3.
10 CAL ARTISAN(MAFUNDI WASHI) WAMEPATIWA MAFUNZO YA KUJENGA NA KUTUMIA MAJIKO SANIFU KUTOKA SHINYANGA MAARIFA CETRE KWA USHIRIKIANO NA KITUO CHA NISHATI MBADALA(TaTEDO) .MAFUNZO YALIFANYAKIA KATIKA KIJIJI CHA BULIMA.
Mafunzo haya yanalenga wanachama wa ALIN na mafundi washi ili kuondokana au kupunguza uharibifu wa mazingira hasa ukataji wa miti kwa ajili ya vyanzo vya nishati
 kwa matumizi ya mkulima kijijini anatumia  mikokoteni mitatu inayovutwa na ng'ombe kwa  hali ambayo ikiendelea kutakuwa na uharibifu  mkubwa wa misitu na kusababisha kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi