Esther Makono:
Nashukuru sana kituo cha maarifa centre kwa mafunzo waliyotupatia ya computer bila gharama yoyote ambapo binafsi yameniwezesha kujua namna ya kuitumia kompyuta na kuniwezesa kutembelea tovuti mbalimbali hasa zihusuzo mambo ya muungu kupitia kanisa letu la Mashahidi wa Yehova(Yehova Witness) mafunzo haya ni gaharama kubwa kuyapata kupitia vyuo vyetu vinavyotoa mafunzo haya ya kompyuta jambo ambalo lilinifanya nishindwe kumudu gharama hizo kutokana na kuwa na watoto wanaosoma vyuoni ambao pia wanahitaji pesa ili waweze kuendelea na masomo yao ,lakini kupitia kituo cha maarifa ambacho kinatoa huduma zake bure nimeweza kupata mafunzo hayo katika program zifuatazo ambazo ni microsoft word,Excel,Power Point pamoja na Internet nashukuru sana.