Wednesday, April 13, 2011

MATUMIZI YA MAJIKO MBADALA

Matumizi ya majiko mbadala ni mradi ambao unasimamiwa na taasisi inayohusika na mpango wa kupunguza gesi ukaa TaTEDO wakishirikiana na taasisi ya misitu mkoani shinyanga Natural Resources Management and Agroforestry Centre (NAFRAC) iliyoko mkoani shinyanga nchini Tanzania ,ambapo jumla ya vijiji 25 vimepatiwa majiko hayo yanayotumia mkaa kidogo na kuni chache hivyo mkuu wa kituo hicho ndg Pastory Mwesiga anatarajia kukutana na wana vijiji hao ili kujua kama majiko wanayowapa kama yanafanya kazi kama walivyo tarajia ,lengo ni kupunguza mabadiliko ya tabia nchi mkoani shinyanga .