Thursday, January 5, 2012

SHINYANGA NA KIWANGO CHA ELIMU TUNACHOKITAKA(SHINYANGA WITH EDUCATION LEVEL WE WANT

Baada ya matokeo mabaya ya mitihani kwa wahitimu wa shule za msingi na sekondari kituo cha kupashana habari SHINYANGA MAARIFA CENTRE kinatoa huduma ya maktaba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa masomo yote bila gharama yoyote hivyo wanafunzi wote mnakaribishwa kwa kukitumia kituo cha maarifa centre tutaongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi mashuleni ukizingatia changamoto nyingi zinazozikabili shule za kata maarufu kama YEBOYEBO .pia kituo cha maarifa centre kinampango wa kupanua wigo katika kuongeza maarifa kwa jamii kwa kuwapatia mafunzo ya kompyuta bila gharama yoyote ile hivyo watu wote mnakaribishwa.

Wednesday, April 13, 2011

MATUMIZI YA MAJIKO MBADALA

Matumizi ya majiko mbadala ni mradi ambao unasimamiwa na taasisi inayohusika na mpango wa kupunguza gesi ukaa TaTEDO wakishirikiana na taasisi ya misitu mkoani shinyanga Natural Resources Management and Agroforestry Centre (NAFRAC) iliyoko mkoani shinyanga nchini Tanzania ,ambapo jumla ya vijiji 25 vimepatiwa majiko hayo yanayotumia mkaa kidogo na kuni chache hivyo mkuu wa kituo hicho ndg Pastory Mwesiga anatarajia kukutana na wana vijiji hao ili kujua kama majiko wanayowapa kama yanafanya kazi kama walivyo tarajia ,lengo ni kupunguza mabadiliko ya tabia nchi mkoani shinyanga .

Monday, May 17, 2010