Wednesday, October 15, 2014

NAMNA KILIMO CHA TUMBAKU KINAVYOATHIRI MISITU SHINYANGA




KILIMO CHA TUMBAKU KINAVYOSABABISHA UKATAJI WA MITI OVYO.
Tumbaku  ni zao la kibishara linalolimwa na kuvunwa ili kutengeneza sigara,kwa mkoa shinyanga zao hili linalimwa kwa wingi wilayani kahama mkoa wa shinyanga.Ambalo pia nizao linaloongoza kwa mapato wilayani kahama ikifatiwa na madini(Dhahabu) yapatikanayo wilayani hapo.
Zao hili baada ya kuvunwa majani yake hukaushwa kwa kutumia majiko yenye kutumia kuni nyingi wakati wa kukausha tumbaku kabla ya kupaki na kuuza kwenye makampuni yanayonunua tumbaku kama ATTT, ALIANCE nk.
Namna tumbaku inavyochangia uharibifu wa misitu:
Baada ya kuvunwa kwa zao hilo la tumbaku wakulima wote hurudisha fikra zao katika msistu wa ushetu ubagwe ulioko wilaya ya ushetu( kahama)mkoa washinyanga ilikupata kuni kwa ajili ya kukaushia tumbaku na badala ya kuvuna kuni wao hutumia fursa hiyo kukata miti mikubwa kwaajili ya kukausha tumbaku pamoja na kuchana mbao kwa ajili ya biashara kinyume na sharia

            

Hii nimitiilyokatwa na kufanywa mbao

Huu ni msitu wa Ushetu Ubagwe ulioko katika wilaya ya Ushetu (Kahama) na hiyondiyo baadhi ya miti inayoendelea kuvunwa na wakulima wa tumbaku ilikupata kuni za kukaushia tumbaku .
Hili ni shimo linalotumika kuchania mbao yaliyochibwa msituni